Habari
DKT. NCHEMBA ATEMBELEA KONGANI YA VIWANDA YA HWTZ SEZ LIMITED ILIYOPO BAGAMOYO MKOANI PWANI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ametembele na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kongani ya Viwanda ya HWTZ SEZ Limited, unaofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani.
DKt. Nchemba amepongeza jitihada zinazofanywa na Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kupitia Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji zaidi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Amesisitiza kuwa uwekezaji ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa DIRA 2050, inayolenga kufikisha uchumi wa Tanzania katika thamani ya dola trilioni moja za Marekani ifikapo mwaka 2050.
Aidha, Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Uwekezaji, Dkt. Fred Msemwa kuhakikisha vijana wanaandaliwa na kupata fursa katika maeneo ya uwekezaji kulingana na taaluma na ujuzi wao, hatua inayolenga kuongeza ajira na kujenga Taifa lenye uchumi imara, shindani na jumuishi.
