Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

PROF. MKUMBO ASHIRIKI JUKWAA LA BLOOMBERG NEW ECONOMY NCHINI INDIA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ameshiriki mzungumzo katika Jukwaa la Bloomberg New Economy lililofanyika New Delhi, India, kama mzungumzaji.

Jukwaa hilo limejadili mabadiliko ya mifumo ya minyororo ya ugavi duniani ambapo katika mjadala huo, Prof.  Mkumbo alisisitiza uwezo na fursa kwa Tanzania kuwa kitovu muhimu cha minyororo ya ugavi kwa Afrika Mashariki na Kati kutokana na nafasi yake ya kimkakati na fursa zilizopo katika biashara, usafirishaji wa mizigo na maendeleo ya viwanda.

Aidha, Prof. Mkumbo aliwahimiza wawekezaji wa kimataifa kutumia fursa zilizopo nchini Tanzania kwa kuwekeza katika sekta mbalimbali za uchumi, akisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika kuimarisha ushindani wa nchi, kukuza biashara na kuchochea maendeleo ya kiuchumi. 

Ushiriki wa Tanzania katika jukwaa hilo ni fursa ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kuitangaza Tanzania  kama eneo lenye fursa za uwekezaji na kiunganishi muhimu cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.PROF. MKUMBO ASHIRIKI JUKWAA LA