Habari
PROF. MKUMBO ATEMBELEA MRADI WA ENEO MAALUMU LA KIUCHUMI BAGAMOYO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ametembelea Mradi wa Eneo Maalum la Kiuchumi Bagamoyo (BSEZ) wenye ukubwa wa hekta 9,800 kujionea maendeleo yaliyofikiwa ndani ya mwaka mmoja.
Katika ziara hiyo ametembelea miradi 6 iliyo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Mradi wa Yintae Electric Tricycle Assembly umepewa ekari 50, unatarajia kuwekeza Dola za Marekani milioni 55 na kuzalisha ajira 200. Mradi wa Sinovest Industry umepewa eneo la mita za mraba 210,080, unatarajia kuwekeza Dola za Marekani milioni 50 na kuzalisha ajira 10,000. Hadi sasa umewekeza Shilingi bilioni 26 na tayari umeanza kutoa ajira ambapo mabinti 139 wameajiriwa katika awamu ya kwanza kwa mafunzo na kazi.
Aidha, Mradi wa HWTZ SEZ Limited umepewa hekta 500 na unatarajiwa kubeba zaidi ya viwanda 150, huku viwanda 7 vikiendeshwa moja kwa moja na mwekezaji huyo. Mradi huo unatarajiwa kuwekeza Dola za Marekani bilioni 1.5 na hadi Septemba 2026 tayari umetumia Dola za Marekani 15,498,990.
Miradi hii inaendelea kuimarisha uzalishaji wa viwanda, kuongeza thamani ya malighafi na kuzalisha maelfu ya ajira kwa Watanzania.
