Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

MKUMBO AKARIBISHA WAWEKEZAJI WA UHOLANZI KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI TANZANIA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,  Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila  Mkumbo, amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Uholanzi kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania, hususajn katika uzalishaji, viwanda, usindikaji na uongezaji thamani.

Akizungumza jijini The Hague tarehe 5 Oktoba 2026, amesema nafasi ya Tanzania kijiografia inaipa fursa ya kuwa kitovu cha uzalishaji na usambazaji wa bidhaa katika masoko ya Afrika.

Prof. Mkumbo amesema Tanzania inalenga kuongeza thamani ya mazao na rasilimali zake ili kuimarisha viwanda, kutengeneza ajira na kupunguza umaskini.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kuimarisha amani na utulivu nchini, huku ushirikiano na Uholanzi ukitoa fursa za kupanua biashara na uwekezaji.

Mkutano huo ni sehemu ya kampeni ya kutangaza fursa za biashara na uwekezaji Tanzania barani Ulaya, iliyoanza tarehe 28 Septemba 2026 nchini Finland, ikaendelea nchini Italia na inayotarajiwa kuhitimishwa nchini Uholanzi tarehe 6 Oktoba 2026. Kampeni hiyo inaandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Ulaya kuelekea Jukwaa la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya litakalofanyika Dar es Salaam mwaka 2027.