Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kuhusu hatua zinazochukuliwa kuratibu na kurahisisha mifumo ya ulipaji kodi na utoaji wa leseni za biashara nchini. Kikao hicho kimefanyika leo, tarehe 19 Oktoba 2026, katika Jengo la Utawala la Bunge, Dodoma.

Katika majadiliano hayo, Kamati imejadili hatua zilizochukuliwa, ikiwemo kuanzishwa kwa mfumo mmoja wa utoaji leseni za biashara na upatikanaji wa taarifa za leseni zinazohitajika katika sekta mbalimbali kupitia tovuti ya TISEZA. Aidha, Kamati imejadili hatua za kuimarisha ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya uwekezaji kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Chaya, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji; Dkt. Fred Msemwa, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Uwekezaji; Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi Mkuu - TISEZA, Bw. Bernard Konga - Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango (ORMU), Bw. Andrew Mahiga - Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji Sekta Binafsi (ORMU).pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.