Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Pius Chaya akijibu swali la Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum.
Akijibu swali hilo, Dkt. Chaya amesema kuwa Serikali inaendelea kutangaza fursa zilizoko kwenye sekta ya kilimo na uchakataji wa mazao kama maeneo ya kipaumbele katika uwekezaji. Katika kilimo cha Chai, mkakati ni kuvutia uwekezaji katika uzalishaji wa chai, uchakataji, ufungashaji, uhifadhi, uongezaji thamani kwa masoko ya ndani na nje.