Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

TAMASHA LA 17 LA KITAALUMA LA MWALIMU NYERERE


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, leo amehudhuria na kutoa hotuba fupi katika Tamasha la 17 la Kitaaluma la Mwalimu Nyerere lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Tamasha hilo pia limehudhuriwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, viongozi mbalimbali wa Serikali, wahadhiri, watafiti, wanafunzi wa vyuo vikuu, wadau wa maendeleo pamoja na wananchi waliojitokeza kushiriki mjadala kuhusu mustakabali wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.

Katika hotuba yake, Mheshimiwa Prof. Mkumbo amesisitiza umuhimu wa dira ya muda mrefu katika kujenga taifa lenye uchumi imara, maendeleo jumuishi, na wananchi wenye uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Aidha, ameeleza kuwa Dira 2050 inalenga kuifanya Tanzania kuwa taifa lenye uchumi wa kisasa unaotegemea maarifa, viwanda, teknolojia, ubunifu, na uwekezaji katika rasilimali watu.

Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya maendeleo kupitia uwekezaji katika elimu, miundombinu, teknolojia ya kidijitali, nishati, pamoja na kuimarisha taasisi za umma kwa ajili ya ustawi wa vizazi vya sasa na vijavyo.