Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

MHE. PROF. MKUMBO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI JUKWAA LA NGAZI YA JUU LA SIASA LA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb) (katikati), katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mussa Azzan Zungu (kulia); Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Tausi Mbaga Kida (kushoto); Balozi wa Tanzania na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Togolani Edris Mavura, pamoja na viongozi wa Serikali na wabunge, katika Ubalozi wa Tanzania, New York, Marekani.

Mhe. Prof. Mkumbo anaongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Jukwaa la Ngazi ya Juu la Siasa la Malengo ya Maendeleo Endelevu (High-Level Political Forum – HLPF) linalofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Katika jukwaa hilo, Mhe. Waziri anatarajiwa kuwasilisha Ripoti ya Hiari ya Nchi ya Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (Voluntary National Review – VNR), Julai 14, 2026 ikiainisha hatua zilizofikiwa ikijusisha mafanikio, uzoefu na hatua zinazofuta za kuongeza kasi ya utekelezaji wa Ajenda 2030.