Habari
PROF. MKUMBO AFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA YA WADAU WA SEKTA YA MILKI, UJENZI, ARDHI NA UWEKEZAJI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, leo amefunga Maonesho ya Kimataifa ya siku tatu ya wadau wa Sekta ya Milki, Ujenzi, Ardhi na Uwekezaji (Tanzania Real Estate Expo- TAREX 2026) yanafanyika kuanzia Novemba 20 hadi 22, 2026, katika ukumbi wa SuperDome uliopo Masaki, Dar es Salaam.
Maonesho hayo yalilenga kuwakutanisha wadau wa sekta ya milki, ujenzi, ardhi na uwekezaji wa ndani na kimataifa ili kujadili fursa na ukuaji wa sekta hiyo nchini Tanzania.
Akifunga Maonesho hayo, Prof. Mkumbo alisema sekta hiyo ni miongoni mwa sekta zenye kuleta mabadikiko makubwa katika kuchangia utekelezaji wa DIRA 2050 kwani inachochea uwekezaji katika sekta nyingine , kukuza ajira na uchumi.
Prof. Mkumbo, alitoa mwito kwa wadau wa sekta ya milki na ujenzi kuzingatie ubora wa kazi, utunzaji wa mazingira na uwekezaji wa pamoja kupitia vyama vya ushirika.
Prof. Mkumbo aliyeambatana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, anayeshughulikia Uwekezaji, Dkt. Fred Msemwa alisisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kuendelea kuiunga mkono sekta binafsi kutoka na mchango mkubwa katika kuchangia uchumi wa dola za Marekani trilioni moja ambapo sekta binafsi itachangia kwa 70%.
Alisema Ofisi yake mratibu wa masuala ya Uwekezaji inaendelea kuweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji huku ikisimamia mipango iliyoimara katika kufikia safari ya nchi ya uchumi wa kati, ngazi ya juu ifikapo mwaka 2050 kama Dira 2050.
