Habari
SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NCHINI ILI KUVUTIA WAWEKEZAJI ZAIDI KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo alipokuwa akifungua jukwaa la majadiliano baina yake na wawekezaji wa kimkakati lililofanyika leo Januari 16, jijini Dar es Salaam.
“Tunahitaji uwekezaji wa ndani na tunahitaji uwekezaji unavutia mitaji kutoka nje” amesema Prof. Mkumbo katika hotuba yake ya ufunguzi akiongeza kuwa “hakuna nchi iliyoendelea bila wananchi wake kushiriki katika ujenzi wa Uchumi, na vile vile, hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na wawekezaji kutoka nje”.
Mheshimiwa Waziri, alieleza kuwa jukwaa hilo ni miongoni mwa hatua za Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na sekta binafsi ili kujenga ushirikiano wa ubia katika kutafuta suluhu zinazokabili shughuli zao badala ya kuwa na pande mbili, upande mmoja ukilalamika na mwingine kutoa majawabu”
Katika uzinduzi wa jukwaa hilo, uliyokwenda sambamba na uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani, Mhe. Waziri ameleza namna Serikali ya awamu ya sita ilivyokusudia kushrikiana na sekta binafsi kufikia malengo ya Dira 2050 ya ujenzi wa taifa lenye Uchumi wa dola trillion moja za Marekali.
Ametoa ufafanuzi kuwa ili kufikia malengo hayo, mpango wa miaka mitano unalenga kukuza uchukumi wa kutoka bilioni 85 kufikia bilioni 118 ifikikapo mwaka 2030 na ukuaji wa Uchumi kutoka asilimia 5.9 za sasa hadi kufikia 10.5.
Ukuaji wa uchumi huo, kwa sehemu kubwa unatarajiwa kuchangiwa na sekta binafsi, ambapo serikali itahakikisha inajenga mazingira wezeshi kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ikijikita katika kuongeza mauzo ya bidhaa nje badala ya malighafi.
Tutavutia wawekezaji watakaojenga si tu viwanda vya uzalishaji, bali tunataka waingize mitambo na teknolojia za kuongeza thamani.
